
JD Vance amesema hatua hiyo ni sawa na tusi na inaenda kinyume na sera za utawala wa Marekanina juhudi za kuhakikisha makubaliano ya amani kati ya Israel na wanamgambo wa Hamas, yaliyosimamiwa na Rais Donald Trump, yanatekelezwa.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Marco Rubio aliyeshutumu hatua hiyo pia, amewaambia waandishi habari kwamba anapanga kuelekea Mashariki ya Kati na kuteua afisa wa kidiplomasia atakayeshirikiana na kamanda wa ngazi ya juu wa Marekani kwenye eneo hilo.
Kwingineko huko The Hague, Mahakama ya Kimataifa ya Haki, ICJ, imesema ni sharti Israel iliruhusu Shirika la Umoja wa Mataifa linalotoa misaada kwa Wapalestina Gaza (UNRWA), kuendelea na shughuli zake za kiutu.