VIWANJANI: “Klabu imeona kwamba bado wanaweza wakatengeneza mazingira ya mashabiki kuingia wakiwa wanatakiwa kulipa pesa”
Mchambuzi wa soka @michaelhyera_ amesema swala la viingilio kwa mashabiki wa Simba SC katika mchezo wa mkondo wa pili wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Nsingizini Hotspurs kutoka Eswatin ni jambo nzuri kulingana na malengo ya klabu hiyo.
Simba tayari ina mtaji wa magoli matatu mkononi walioyapata kwenye mchezo wa mkondo wa kwanza nchini Eswatini.
Mechi hii itapigwa katika dimba la Benjamin Mkapa kuanzia saa 10:00 jioni na itakuwa LIVE AzamSports1HD.
Imeandikwa na @davidkyamani
Mhariri: @allymufti_tz
#Viwanjani