VIWANJANI | “kumuona Shomari Kapombe kwenye tuzo hii, inabakia kuwa ni heshima kwa Shomari Kapombe”
Mchambuzi wa soka @michaelhyera_ amesema kumuona Shomari Kapombe wa Simba SC, kwenye kinyang’anyiro cha kumsaka Mchezaji Bora wa mwaka wa CAF ni jambo jemba na limechangiwa na kiwango cha mchezaji huyo msimu uliopita.
Kwa upande wa @akingamkono amesema kwa sasa imeanza kujenga kama tabia kwa wachezaji kutoka timu za Tanzania kuingia katika kinyang’anyiro hiko akimtaja na Djigui Diarra wa Yanga.
Imeandikwa na @jairomtitu3
Mhariri: @allymufti_tz
#Viwanjani