WAJIBU WA MASHABIKI WA YANGA: “Nafikiri kwenye swala la mashabiki wao sasa ni kama Yanga imewapa deni wao”

WAJIBU WA MASHABIKI WA YANGA: “Nafikiri kwenye swala la mashabiki wao sasa ni kama Yanga imewapa deni wao”
Mchambuzi wa soka @michaelhyera_ viongozi wa Yanga wametekeleza wajibu wao kwa kuondoa viingilio kwenye mchezo wa Jumamosi dhidi ya Silver Strikers.

Hyera anasema sasa imesalia kazi kwa mashabiki wa timu hiyo kuhakikisha Jumamosi wanakwenda kuwapa hamasa wachezaji ili kuweza kupata matokeo mazuri.

Kwa upande wake mchambuzi wa soka @akingamkono amesema uongozi wa Yanga SC unatakiwa kuweka utaratibu nzuri ili kuimarisha ulinzi na usalama wa uwanja kutokana na wingi wa mashabiki watakaojitokeza kwenye mchezo huo.

Mechi hiyo itapigwa kuanzia saa 11:00 jioni katika dimba la Benjamin Mkapa na itakuwa LIVE AzamSports3HD.

Imeandikwa na @davidkyamani
Mhariri: @allymufti_tz

#Yanga

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *