Wananchi wameshauriwa kutumia kura zao kama njia sahihi ya kuonesha maoni na kufanya maamuzi katika uchaguzi mkuu utakaofanyika …Wananchi wameshauriwa kutumia kura zao kama njia sahihi ya kuonesha maoni na kufanya maamuzi katika uchaguzi mkuu utakaofanyika …

Wananchi wameshauriwa kutumia kura zao kama njia sahihi ya kuonesha maoni na kufanya maamuzi katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 29, 2025, badala ya kushiriki maandamano ambayo mara nyingi husababisha madhara kwa jamii na taifa.

Hayo yamebainisha na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Vijana na Wanawake (TAFEYOCO), Elvis Makumbo wakati akizungumzia utafiti wa maoni ya wananchi waliofanya katika Mikoa ya Dar Es Salaam na Pwani kuhusu mwelekeo wa uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oct 29 2025.

Amesema badala ya kufikiria maandamano, wananchi wanapaswa kusikiliza kwa makini sera za wagombea wa vyama mbalimbali na kisha kufanya maamuzi katika sanduku la kura.

Kupitia mkutano huo wananchi wameshauriwa kijiepusha na fikra za kutaka kuleta vurugu na kuharibu amani ya nchi badala yake wajitoleze kupiga kura bila kuhofia maneno ya mitandaoni.

Tayari Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) imetangaza kuwa uchaguzi mkuu wa mwaka 2025, utakaohusisha nafasi ya Rais, wabunge na madiwani, utafanyika siku ya Jumatano, tarehe 29 Oktoba 2025 na hivyo watanzania wametakiwa kujitokeza kwa wingi kupiga kura ili kuchagua viongozi watakaowaletea maendeleo kwa miaka mitano.

Mwisho

#StarTvUpdate

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *