.

Chanzo cha picha, UDASA

Jumuiya ya wanataaluma wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDASA) nchini Tanzania imetoa tamko la kusikitishwa kwakwe na matukio ya watu kupotea au kudaiwa kutekwa, kikisema hali hiyo inatishia uhuru wa kujieleza na misingi ya haki za binadamu nchini.

Katika taarifa yake, UDASA imesema matukio hayo yamezua hofu miongoni mwa wananchi na kuathiri taswira ya taifa katika jamii ya kimataifa.

Jumuiya hiyo imeitaka serikali na vyombo vya usalama kuchunguza kwa uwazi na kwa haraka visa vyote vya aina hiyo ili kutoa majibu ya kweli kwa umma.

Tamko hilo limerejea ripoti ya shirika la haki za binadamu (LHRC) kuhusu tishio la kile kinachoidwa “Watu wasiojulijkana” wakilitupia lawama Jehsi la Polisi kwa ama kushindwa kudhibiti au kutolea ufafanuzi.

Hata hiyo mara kadhaa Jeshi la Polisi limeeleza kuendelea kufuatilia wanaodaiwa kutekwa, na lilishawahi kukanusha kutohusika na wapo wengine waliodaiwa kutekwa kubainika kujiteka.

Kuhusu idadi ya waliotekwa ama kupoktea, tamko la UDASA limerejea tena ripoti ya LHRC waliobainisha kati yam waka 2021 mpaka 2024 watu 87 wametekwa na kupotezwa.

Mbunge wa zamani wa CCM na Askofu Josephat Gwajima aliwahi pia kudai kwamba watu zaidi ya 83 waliripotiwa kutekwa au kupotea katika kipindi hicho.

UDASA pia imewataka viongozi wa serikali, vyama vya siasa na wadau wengine kulinda haki ya kujieleza bila woga wa vitisho au madhara, ikisisitiza kuwa uhuru huo ni nguzo muhimu katika maendeleo ya demokrasia.

Katika tamko hilo, Jumuiya hiyo imeeleza umuhimu wa kujenga mazingira salama kwa wahadhiri, wanafunzi na wanaharakati kushiriki mijadala ya kitaaluma na kijamii bila kuonewa au kudhibitiwa.

UDASA imesema bila uhuru huo, misingi ya utawala bora inaweza kudhoofika.

Aidha, chama hicho kimehimiza serikali kuchukua hatua madhubuti kuhakikisha vyombo vya dola vinawajibika ipasavyo na kwamba kila raia anatendewa haki bila upendeleo.

Hata hivyo, Serikali ya Tanzania mara kadhaa imekanusha kuhusika kwa namna yoyote na vitendo vya utekaji au kupotea kwa watu.

Vilevile, Jeshi la Polisi limesema kumekuwa na matukio ambapo baadhi ya watu waliodai kutekwa baadaye walithibitishwa kujiteka wenyewe na kuongeza kuwa linaendelea kufuatilia kila taarifa inayotolewa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *