Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ameagiza kituo cha polisi Nandagala kilichopo Wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi kianze kutoa huduma ifikapo Novemba Mosi mwaka huu.

Akikagua ujenzi wa kituo hicho leo, Majaliwa amesema majengo yamekamilika na amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Ruangwa, Frank Chonya, kuhakikisha samani zinawekwa mara moja.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Lindi, ACP John Imori, amesema ujenzi wa kituo hicho cha daraja C umegharimu shilingi milioni 194.3 na umefikia asilimia 95 ya utekelezaji.

Amesema utekelezaji huo ulifanyika kwa mfumo wa force account na fedha zilizookolewa zimetumika kujenga nyumba mbili za maafisa wa polisi.

Kukamilika kwa kituo hicho kutawezesha wananchi wa vijiji 32 katika kata nane kupata huduma za usalama kwa urahisi zaidi.

#AzamTVUpdates
✍ Warda John
Mhariri | @claud_jm

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *