Waziri wa Usalama wa Taifa wa Iran amesema kuwa Jamhuri ya Kiislamu haina imani kabisa kuhusu kulindwa maslahi ya nchi hii kupitia kufanya mazungumzo na Marekani.

“Hatuna imani na mazungumzo yoyote na Marekani ambayo yanadai kulinda maslahi yetu ya taifa,” amesema Esmaeil Khatib Waziri wa Usalama wa Taifa wa Iran katika mkutano jana Jumatano mkoani Chaharmahal na Bakhtiari magharibi mwa Iran.

Khatib ameeleza kuwa, madai ya Washington kwamba inaendeleza mazungumzo na Iran yanaficha “uhasama wake dhidi ya taifa la Iran.”

Waziri wa usalama wa Taifa wa Iran amezungumzia pia njama kubwa zilizofanywa na Marekani, utawala wa Israel na nchi nyingine maadui wa Iran ili kuibua uasi, kuzusha machafuko na kuisambaratisha nchi wakati wa vita vya siku 12 vya mwezi Juni mwaka huu vilivyoanzishwa na Washington na Tel Aviv dhidi ya Tehran.   

Esmaeil Khatib ameeleza namna njama za chokochoko hizo zisizo na msingi zimekuwa zikitekelezwa na maadui kwa mika mingi dhidi ya Iran ili kuitenga nchi hii kupitia propaganda kubwa, kuifanya dunia iwe dhidi ya Iran na kuwatoa watu katika Mapinduzi ya Kiislamu.  

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *