
Mahakama ya Afrika Kusini imempa rais wa zamani Jacob Zuma siku 60 za kulipa zaidi ya Euro milioni 1. Mkuu huyo wa zamani wa nchi, kiongozi wa ufisadi na kashfa zingine serikali nchini Afrika Kusini, aliyelazimishwa kuondoka madarakani mwaka wa 2018, amepatikana na hatia ya kutumia pesa za umma kwa ada zake za kisheria.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Na mwandishi wetu jijini Johannesburg, Valentin Hugues
Kwa mara ya kwanza, mahakama ya Afrika Kusini imetoa kauli ya mwisho kwa rais wa Zamani Jacob Zuma: mkuu huyo wa zamani wa nchi, aliyepatikana na hatia ya kutumia pesa za umma kwa ada zake za kisheria, ana miezi miwili ya kulipa zaidi ya Euro milioni 1.
Kesi hii si mpya; mahakama imekuwa ikifanya kazi katika suala hili la pesa za umma kutumika kwa masuala ya kisheria ya kibinafsi kwa miaka kadhaa. Mnamo mwaka 2021, mbele ya Mahakama ya Rufaa, mawakili wa Jacob Zuma walitumia dhana ya dhima, wakidai kwamba rais huyo wa zamani wa Afrika Kusini hakuwa na jukumu “kibinafsi”. Lakini mahakama haikubaliani hoja hiyo. Mahakama Kuu ya Pretoria iimetangaza kwamba Jacob Zuma ana hatia kweli, akiwajibika kwa kutumia fedha za serikali kinyume cha sheria kwa ada za kisheria zinazohusiana na kesi zake za ufisadi binafsi.
Siku 60 za kulipa pesa yote
Jacob Zuma sasa ana siku 60 za kulipa kiasi kilichoombwa, ikishindikana pensheni yake ya zamani ya rais inaweza, kwa mfano, kuzuiwa. Rais huyo wa zamani amezungumzia kuhusu uamuzi huu, lakini hoja yake haieleweki. “Mkutano umepangwa na mawakili wangu kujadili hatua zinazofuata katika suala hili. Tumepanga kukutana nao ili kuendeleza suala hili,” alisema.
Chama cha pili kwa ukubwa cha siasa nchini Afrika Kusini kimekaribisha uamuzi huu. “Tunatarajia kumuona Bw. Zuma akilipa kile anachodaiwa Afrika Kusini,” Muungano wa Kidemokrasia uliandika katika taarifa.