Baadhi ya abiria waliokuwa wakisafiri kwa treni za SGR kati ya Dar es Salaam na Dodoma wamesema wamefarijika kuona huduma za usafiri wa reli hiyo kurejea muda mfupi baada ya ajali iliyotokea eneo la Ruvu, mkoani Pwani, Oktoba 23, 2025.

Wakizungumza katika vituo vya Dar es Salaam, Morogoro na Dodoma, abiria hao wamesema walidhani safari zingesitishwa kwa muda mrefu kutokana na ajali hiyo.

Awali, ajali hiyo ilisababisha usumbufu kwa muda mfupi katika ratiba za safari, huku Shirika la Reli Tanzania (TRC) likitoa taarifa kuwa huduma zimeanza tena baada ya ukarabati wa eneo lililoathirika kukamilika.

✍ Mwandishi Wetu
Mhariri @claud_jm
#AzamTVUpdates

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *