Wananchi wa Cote Dvoire, kesho watapiga kura kwenye uchaguzi mkuu ambao rais Alassane Ouattara, anatarajiwa kushinda muhula wa nne, baada ya wapinzani wake wakuu rais za zamani Laurent Gbagbo na mwanasiasa mashuhuri wa upinzani Tidjane Thiam kuzuiwa kushiriki.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Rais  Ouattara, mwenye umri wa miaka 83, anakabiliwa na upinzani kutoka kwa wagombea wengine wanne, wanaonekana kutokuwa tishio, kubwa baada ya kuondolewa kwa Gbagbo na Thiam, kwa sababu hawakujiandikisha kama wapiga kura kwa mujibu wa Mahakama ya Katiba.

Siku ya Jumatano, Gbagbo alisema uchaguzi wa Jumamosi ni kama mapinduzi ya kiraia na tayari wizi wa kura umeshafanyika, kumpa ushindi rais Ouattara, ambaye amekuwa madarakani tangu mwaka 2011.

Ouattara, amekuwa akiwaambia wananchi wa taifa hilo la Afrika Magharibi kuwa, moja ya sababu ya kutaka kuendelea kuongoza ni kwa sababu ya kutaka kuimarisha uchumi wa nchi hiyo tangu alipoingia madarakani.

Watu Milioni nane, wamendikishwa kwenye dafatri la kupigia kura, lakini kwa mazingira ya kisiasa, yaliyopo, wachambuzi wa siasa wanaona kuwa, huenda idadi kubwa ya wapiga kura wasijitokeze kushiriki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *