Viongozi hao wameweka masharti ikiwemo kuacha nafasi ya makubaliano hayo kupitiwa upya tena katika siku zijazo.

Hakuna uamuzi wa mwisho uliofikiwa na hakutarajiwi uamuzi, ila mazungumzo hayo ya viongozi hao yanatarajiwa kutoa mwelekeo wa makubaliano ndani ya wiki mbili zijazo.

Viongozi wa mataifa 27 ya Umoja wa Ulaya wamefanya mazungumzo mjini Brussels kujaribu kupata mwafaka kutokana na malengo yao kadhaa waliyo nayo, ambayo ni kuunga mkono biashara za umoja huo zinazodorora ikiwemo sekta ya magari na kwa upande mwengine, kuongoza katika mapambano dhidi ya mabadiliko ya tabia nchi.

Mkutano huo unafanyika wakati ambapo Umoja wa Ulaya unakabiliwa na shinikizo la lengo lao kubwa la kupunguza utoaji wa gesi chafu kuelekea mkutano mkuu wa mazingira wa Umoja wa Mataifa utakaofanyika nchini Brazil mnamo Novemba 10.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *