
Hadi sasa, idadi ya vivuko haramu kwenye bahari Manche imezidi ile ya mwaka mzima wa 2024. Karibu watu 37,000 wamewasili kwenye fukwe za Uingereza, wakiwa ndani ya boti ndogo zinazoondoka pwani ya Ufaransa.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Hiki ni kikwazo kwa serikali ya Uingereza, ambayo ilisaini makubaliano ya uhamiaji na Ufaransa mwezi Julai mwaka huu, yaliyokusudiwa kuwazuia wahamiaji kuingia baharini. Inafuata kanuni ya “mmoja kwa mmoja”, huku idadi sawa ya wakimbizi waliorudi Ufaransa kama ilivyokubaliwa kisheria katika ardhi ya Uingereza. Lakini makubaliano haya, ambayo yamekosolewa sana kimsingi, bado hayajaonyesha ufanisi wake.
Tangu makubaliano haya ya uhamiaji yaanze kutumika, wahamiaji 42 pekee wamehamishwa kwenda Ufaransa na 23 wamepewa visa nchini Uingereza. Kulingana na Nigel Farage, kiongozi wa chama cha mrengo wa kulia cha Reform UK makubaliano hayo yameshindwa kabisa.
Hasa tangu raia wa Iran, aliyehamishwa kwenda Ufaransa, alipovuka Channel tena siku chache zilizopita. Maafisa waliochaguliwa kaskazini mwa Ufaransa pia wanalaani makubaliano yasiyofaa kabisa, kama meya wa Sangatte, karibu na Calais, Guy Allemand, alivyomwambia Marie Casadebaig wa RFI.
“Makubaliano haya ya pande mbili hayafanyi chochote kuhakikisha usalama wa wahamiaji au kujaribu kuwaangamiza wasafirishaji haramu katika mitandao yao ya mafia. Ni makubaliano ya kisiasa tu, amesema, akiongeza na makubaliano haya ni ya kinafiki sana. Unapoona idadi hiyo ikirudishwa kwetu na ile inayopaswa kuondoka, ni sehemu ndogo ya makumi ya maelfu ya majaribio yaliyofanikiwa. Wahamiaji hawakatishwi tamaa kwa njia yoyote.”
Nchini Ufaransa, Baraza la Nchi linatarajiwa kutoa uamuzi hivi karibuni. Mashirika yasiyo ya kiserikali kumi na tano yamewasilisha malalamiko kwa mahakama ya juu zaidi katika jaribio la kufuta makubaliano haya, yakilaani kanuni zake zisizo za kibinadamu. Tangu Januari 1, 2025, njia wanazotumia wahamiaji kwa kuh=vuka Bahari Manche zimesababisha vifo vya watu wasiopungua 27, kulingana na hesabu ya shirika la habari la AFP.