Chanzo cha picha, Getty Images
Baada ya kuwa na safu bora ya ulinzi, lakini wakifunga kiwango cha chini cha mabao 17 pekee ikilinganishwa na mabingwa Liverpool msimu uliopita, ilionekana dhahiri Arsenal ingelazimika kuboresha safu yao ya mashambulizi ikiwa wangepata nafasi nzuri ya kushinda Ligi ya Premia wakati huu.
Lakini kwa kufungwa mara tatu pekee katika mechi nane za mwanzo msimu huu – na kuongoza ligi kwa pointi tatu wakiwa nafasi ya kwanza – safu yao ya ulinzi tayari imeimarika hadi kufikia kiwango cha kihistoria na huenda wasihitaji kufunga mabao mengi zaidi.
Ni jambo zuri pia kwa sababu, wakati safu ya ushambuliaji ya The Gunners ni bora kuliko ilivyokuwa msimu uliopita, bado ina changamoto ya kushinda ubingwa msimu wa 2023-24 walipofunga wastani wa mabao 2.4 kwa kila mechi.
Safu ya ulinzi ya Arsenal imeimarika sana msimu huu
Chanzo cha picha, Getty Images
Huku Martin Odegaard, Noni Madueke, Gabriel Jesus na Kai Havertz wakiwa miongoni mwa wachezaji wabunifu ambao kwa sasa hawana majeraha, safu ya ushambuliaji ya Arsenal inaweza kuimarika kadri msimu unavyoendelea.
Lakini ikiwa haitafanya hivyo, je ulinzi wao utatosha kunyanyua kombe la ligi kuu kwa mara ya kwanza tangu 2004?
Kati ya timu 33 zilizoshinda Ligi Kuu, ni sita pekee ndizo zimeshinda zikiruhusu mabao machache zaidi na kutofunga mabao mengi (18%).
Timu ya mwisho kufanikiwa kwa mtindo kama huo ilikuwa Liverpool ya Jurgen Klopp mnamo 2019-20, ambayo ilimaliza subra ya miaka 30 licha ya kufunga mabao 17 pekee kuliko magoli 102 ya Manchester City msimu huo.
Mabingwa sita wa Premier League wameshinda taji hilo kwa kuwa na safu bora ya ulinzi
Lakini Arsenal wamekuwa na safu bora ya ulinzi katika misimu miwili iliyopita na bado walimaliza nafasi ya pili, kwa hivyo ni nini kinachoweza kuwa tofauti wakati huu?
Ingawa bado mapema, hatuangalii tu kuwa na safu bora ya ulinzi msimu huu lakini mojawapo ya bora zaidi katika kampeni zozote za Ligi Kuu.
Kiwango chao cha sasa cha kufungwa mabao 0.38 pekee kwa kila mechi kinamaanisha iwapo wangedumisha hilo kwa msimu mzima, wangeruhusu mabao 14 pekee na kuvunja rekodi ya ajabu ya mabao 15 iliyowekwa na kikosi cha Chelsea kilichoshinda taji la Jose Mourinho mnamo 2004-05.
Kwa kweli, kwa kiwango chao cha sasa cha kufunga mabao 1.88 kwa kila mchezo, vijana wa Mikel Arteta wako mbioni kuakisi timu hiyo ya ajabu, ambayo inaweza kufunga mara 71 na kufungwa 14, ikilinganishwa na jumla ya mabao 72 na 15 ya Chelsea.
Hiyo itamaanisha Arsenal kufunga mabao mawili zaidi ya 69 msimu uliopita, lakini wakiruhusu mabao 20 pekee ikilinganishwa na mabao 34 mara ya mwisho.
Kwa kuwa washindi wa Ligi Kuu kwa wastani wamefunga mabao 84 na kuruhusu 32 katika msimu wa mechi 38, kiwango chao cha sasa kinaweza kuwafanya kuwa mabingwa wasioweza kuyumbishwa, badala ya wasiozuilika, katika historia.
Arsenal wako mbioni kuiga Chelsea ambayo haikuweza kushindwa msimu wa 2004-05
Hatahivyo, ingawa Arsenal imekuwa ikivutia sana, ikilinganishwa na safu ya ulinzi ya Chelsea miaka 20 iliyopita itakuwa kazi ngumu kuafikia.
Kwa kuanzia, wanahitaji kutofungwa magoli katika mechi zao tatu zijazo dhidi ya Crystal Palace, Burnley na Sunderland ili tu kufikia mabao matatu ambayo Chelsea walikuwa wameruhusu baada ya mechi 11.
Si hivyo tu, lakini sababu kubwa iliyowafanya vijana wa Mourinho kuruhusu 15 pekee msimu huo ni kwa sababu, baada ya kufungwa mara mbili katika sare ya 2-2 na Arsenal mnamo 12 Desemba 2004, hawakuruhusu mabao mengine kwenye ligi hadi Machi 5, 2005, wakati wa ushindi wa 3-1 dhidi ya Norwich.
Hiyo ilimaanisha Chelsea walikuwa wamefungwa mara nane pekee katika mechi 27.
Chanzo cha picha, Getty Images
Je, Arsenal inaweza kuipiku rekodi ya Chelsea ya kutofungwa kwa kuruhusu mabao 15 pekee?
Mkimbio huo wa mechi 10 mfululizo za ligi bila kufungwa uliweka rekodi wakati huo, lakini baadaye ulivunjwa na Manchester United ya mechi 14 mnamo 2008-09.
Kati ya Januari 31 na Machi 31, 1998, Arsenal walicheza mechi nane bila kufungwa wakiwa njiani kunyanyua taji lao la kwanza la Premier League chini ya Arsene Wenger.
Kikosi cha Arteta kitalazimika kufikia rekodi hiyo – au hata kushinda – wakati fulani ikiwa watategemea ulinzi wao katika kuwaongoza kuibuka washindi mwezi Mei.