
Jeshi hilo halikusema ni kundi gani lilihusika na mashambulizi hayo lakini duru za kijasusi zimeliambia shirika la habari la AFP kwamba wanamgambo wa ISWAP walihusika.
Msemaji wa Jeshi Luteni Kanali Sani Uba, amesema katika taarifa kwamba juhudi za pamoja za vikosi vya ardhini na angani zilisababisha kuuawa kwa magaidi hao.
Uba ameongeza kuwa mashambulizi hayo ya ardhini na angani bado yanaendelea kuwasaka zaidi ya waasi 70 waliojeruhiwa.
Makumi ya silaha na maguruneti zanaswa
Afisa huyo amesema wanajeshi wamenasa makumi ya silaha na maguruneti kutoka kwa wanamgambo hao.
Pia ameongeza kuwa wanajeshi kadhaa wamejeruhiwa katika mapigano hayo bila ya kutoa idadi kamili.
Waasi wenye silaha Afrika Magharibi wanazidi kutumia droni, mara nyingi za miundo ya kibiashara iliyorekebishwa kurusha mabomu au maguruneti.