
Kwa mujibu wa chanzo cha karibu na mazungumzo hayo chini ya mwavuli wa Quad, mkutano huo utajadili njia za kuzitaka pande zinazopigana kuheshimu usitishaji vita wa miezi mitatu uliopendekezwa kote nchini Sudan.
Kundi hilo la Quad pia linafanya juhudi za pamoja kuhakikisha misaada ya kibinadamu inafika kwa waathiriwa wa mapigano.
masuala yanayoshinikizwa na Quad
Chanzo hicho kimeeleza kuwa wawakilishi wa mataifa hayo manne watakutana na pande hizo kwa nyakati tofauti.
Mwezi uliopita, Quad ilitoa wito wa kusitishwa kwa mapigano, kuruhusu misaada kuingia Sudan humo, na kuweka msingi wa usitishaji wa kudumu wa vita pamoja na mpito kuelekea utawala wa kiraia.