Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), imesema kuwa Kimbunga Chenge kimeendelea kusalia baharini na kusogea Magharibi (Pwani ya Tanzania).
Taarifa ya Mamlaka hayo iliyotolewa leo Ijumaa Oktoba 24,2025 imesema kuwa, hadi kufikia asubuhi ya leo Kimbunga Chenge kilikuwa katika eneo la Bahari ya Hindi umbali wa takribani kilometa 1,680 Mashariki mwa Pwani ya Mtwara.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, uchambuzi wa mifumo ya hali ya hewa inaonyesha kuwa kimbunga hicho kinatarajiwa kuendeleae kusogea kuelekea Magharibi zaidi mwa Bahari ya ulipo ukanda wa pwani wa nchi yetu huku kikipungua nguvu yake kadri kinavyosogea.
#StarTvUpdate
