
Trump ataanza ziara kubwa ya kidiplomasia barani Asia, Oktoba 30 kwa mkutano wa maamuzi na Rais wa China Xi Jinping nchini Korea Kusini.
Imechapishwa:
Dakika 2 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Donald Trump anajiandaa kuanza ziara ndefu barani Asia, ikifikia kilele chake katika mkutano unaotarajiwa sana na Rais wa China Xi Jinping, uliopangwa kufanyika Oktoba 30 nchini Korea Kusini. Mkutao huu ni muhimu kwa uchumi wa dunia, kwani mataifa hayo mawili yanatafuta kupunguza mvutano wao wa kibiashara huku yakifafanua upya usawa wao wa nguvu. Rais wa Marekani ameonyesha matumaini yake: anatumai kuhitimisha “makubaliano mazuri” na Beijing na kujadili “kila kitu,” kuanzia biashara hadi mizani ya kimkakati katika eneo hilo.
Kwa mujibu wa Ryan Hass, mtafiti katika shirika la Marekani la Brookings, mkutano huu hautarajiwi kuwa “hatua kubwa ya mabadiliko” katika uhusiano kati ya China na Marekani. Donald Trump pia atakutana kwa mazungumzo na Rais wa Korea Kusini Lee Jae Myung, atatoa hotuba kwa viongozi wa biashara, na kuhudhuria chakula cha jioni rasmi cha viongozi wa APEC, mkutano wa kilele wa Ushirikiano wa Kiuchumi wa Asia na Pasifiki. Suala la Korea Kaskazini, lililofufuliwa upya na uzinduzi wa makombora ya hivi karibuni, pia litakuwa kwenye ajenda. Rais wa Marekani amebainisha tena nia yake ya kukutana na Kim Jong Un tena “labda mwaka huu.”
Lakini kabla ya hapo, rais wa Marekani atasimama huko Malaysia, ambapo atashiriki katika mkutano wa kilele wa Jumuiya ya Mataifa ya Kusini-mashariki mwa Asia (ASEAN), kuanzia Oktoba 26 hadi 28 huko Kuala Lumpur. Donald Trump, ambaye alisisia tukio hili wakati wa muhula wake wa kwanza, anapanga kuhitimisha makubaliano ya biashara ya pande mbili na kushuhudia kusainiwa kwa mkataba wa amani kati ya Thailand na Cambodia, nchi mbili hivi karibuni zikitoka kwenye migogoro kutokana na upatanishi wake.
Mnamo Oktoba 29, Donald Trump atasafiri kwenda Japani kukutana na Waziri Mkuu Sanae Takaichi, mkuu mpya wa serikali na mwanamke wa kwanza kushikilia wadhifa huo. “Tutakuwa na majadiliano ya wazi,” Sanae Takaichi amesema, akionyesha nia yake ya kuimarisha uhusiano wa kibiashara na Washington. Kwa pamoja, wanatarajiwa kujadili masuala kadhaa, ikiwa ni pamoja na uagizaji wa nishati ya Urusi na matumizi ya ulinzi wa Japai. Ziara hii ya Asia, ya kwanza tangu aliporejea madarakani mwezi Januari, inaonekana kuwa fursa ya kidiplomasia yenye hatari kubwa, lakini pia kuonyesha ushawishi.