Mgombea wa urais wa Tanzania kwa tiketi ya CCM, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameahidi kuulinda na kuudumisha Muungano wa Tanzania Bara na Zanzibar kwa nguvu zake zote, akisema muungano huo umeleta manufaa makubwa kwa pande zote mbili.
Akizungumza kwenye mkutano wa kampeni katika Viwanja vya Mnazi Mmoja, Unguja, Dkt. Samia amesema serikali ijayo ya CCM itaendeleza maendeleo jumuishi kwa kuboresha huduma za kijamii ikiwemo elimu, maji, na umeme.
Amesema yeye na Dkt. Mwinyi wamejipanga kuhakikisha Zanzibar inapata umeme wa uhakika saa 24 kwa siku, siku saba kwa wiki.
Aidha, ameahidi kuimarisha uchumi kupitia uwezeshaji wa vijana na wanawake, kukuza ajira na kuendeleza sekta za viwanda, kilimo, utalii na uchumi wa buluu.
✍ @claud_jm
#AzamTVUpdates