Mkurugenzi mstaafu wa makosa ya jinai( DCI) na mbunge wa zamani wa jimbo la Muheza Mkoani Tanga, Balozi Adadi Rajabu amewatoa hofu Watanzania kwamba hakutakuwa na maandamano siku ya tarehe 29 hivyo wajitokeze kwa wingi kwa ajili ya Kwenda kutekeleza haki yao ya kikatiba ya kupiga kura.
Balozi Adadi ametoa kauli hiyo wakati wa mkutano wa kampeni kwa ajili ya kumuombea kura Rais Samia Suluhu Hassan Pamoja na mbunge wa Muheza hamis Mwijuma maarufu (Mwanafa)uliofanyika katika kaya ya Nkumba wilayani Muheza.
#StarTvUpdates
