Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Abubakar Kunenge ameutaka Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) kuongeza uwekezaji wa nyumba na majengo ya ofisi mkoani humo ili kukidhi mahitaji yanayoongezeka kutokana na uwepo wa zaidi ya viwanda 1,600.
Ametoa wito huo wakati akipokea msafara wa Mkurugenzi wa Idara ya Miliki kutoka TBA, akisisitiza kuwa uwekezaji zaidi utasaidia kuboresha makazi na kuvutia wawekezaji wapya katika sekta ya viwanda.
#AzamTVUpdates
✍ Upendo Michael
Mhariri | John Mbalamwezi