Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Paul Chacha, amesema Watanzania wanapaswa kujivunia amani waliyonayo na tusiipoteze kirahisi

Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Paul Chacha, amesema Watanzania wanapaswa kujivunia amani waliyonayo na tusiipoteze kirahisi.

Badala yake mkuu huyo wa mkoa ametaka Watanzania kudumisha amani na mshikamano, akisisitiza kuwa amani ni tunu muhimu ambayo ikipotea ni vigumu kuipata tena.

Akizungumza katika mkutano uliowakutanisha viongozi wa dini na waumini wa madhehebu mbalimbali mkoani Tabora, Chacha amesema Tanzania ni nchi iliyobarikiwa kuwa na utulivu wa kudumu.

“Tangu mwaka 1972, Tanzania imeendelea kuwahifadhi wakimbizi kutoka mataifa jirani kama Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, jambo linalodhihirisha moyo wa upendo, utu na haki uliopo nchini huku akibainisha kuwa Watanzania hawapaswi kudanganyika na maneno ya uchochezi au ushawishi wa kuvuruga umoja wa Taifa,” amesisitiza mkuu huyo wa mkoa.

#StarTvUpdate

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *