Dar es Salaam. Rais Samia Suluhu Hassan ametangaza Jumatano Oktoba 29, 2025 kuwa siku ya mapumziko ya kitaifa ili kuwawezesha Watanzania kushiriki katika shughuli ya kupiga kura.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Dk Moses Kusiluka, jana Oktoba 24, 2025, imeeleza kuwa uamuzi huo umetolewa baada ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) kutangaza siku hiyo kuwa siku ya uchaguzi mkuu wa rais, wabunge na madiwani.

“Kwa madhumuni ya kuwawezesha wananchi wenye sifa stahiki, wakiwemo watumishi wa umma na wafanyakazi wa sekta binafsi, kutumia haki yao ya kikatiba ya kupiga kura, Rais amethibitisha Oktoba 29, 2025 kuwa siku ya mapumziko,” imeeleza taarifa hiyo.

Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi tayari imetoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi siku hiyo na kutumia haki yao ya kidemokrasia kuchagua viongozi watakaowaongoza kwa miaka mitano ijayo.

Endelea kufuatilia Mwananchi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *