
Shirika hilo limesema Kongo inakabiliwa na mojawapo ya majanga makubwa na yaliyosahaulika ya kibinadamu duniani na kwamba hali inaendelea kuwa mbaya zaidi.
Oxfam, pia imesema unyanyasaji wa kijinsia umefikia viwango vya kutisha, huku mwanamke mmoja akibakwa kila baada ya dakika nne.
Msaada wa kimataifa wapungua
Hata hivyo licha ya hali hiyo ya dharura, msaada wa kimataifa unapungua.
Oxfam, imesema katika muda wa mwaka mmoja, ufadhili wa misaada muhimu umepungua kwa thuluthi mbili nchini Kongo na imelihimiza kongamano la kimataifa kuhusu Kanda ya Afrika ya Maziwa Makuu, linaotarajiwa kufanyika nchini Ufaransa Oktoba 30, kuchukuwa hatua zaidi ya matamko ya nia.