Kulingana na afisa aliye karibu na nchi hizo nne, mkutano huo utakuwa unalenga kuzipatanisha pande hizo mbili zilizo kwenye mzozo ili zisitishe mapigano.

Mwezi uliopita nchi hizo za kigeni zenye ushawishi kwa pamoja zilitoa mwito wa usitishwaji wa mapigano kwa ajili ya kutolewa kwa msaada wa kiutu, kisha baada ya hapo usitishwaji kamili wa mapigano ufuatie, hatua itakayofungua njia ya utawala wa kiraia.

Afisa huyo mwandamizi ameliambia shirika la habari la Ufaransa AFP kuwa mkutano huo wa wiki hii pia una lengo hilo na kuzishinikiza pande hizo mbili zinazozozana kusitisha mapigano kwa miezi mitatu kwa ajili ya misaada ya kiutu.

Afisa huyo amesema wawakilishi wa pande hizo watakutana na wawakilishi wa mataifa hayo mane katika mikutano miwili tofauti.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *