Photos from Habari Star TV Tanzania's post

Rais Samia Suluhu Hassan ametangaza Oktoba 29,2025 kuwa siku ya mapumziko ili kutoa fursa kwa wanaanchi kushiriki katika Uchaguzi Mkuu.

Taarifa ya Ikulu iliyosainiwa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Dkt Moses Kusiluka imesema kuwa Rais Samia ametumia Mamlaka aliyonayo chini ya Sheria ya Sikukuu za Kitaifa sura ya 35.

Kwa mujibu wa Katibu Mkuu Kusiluka, madhumuni ni kuwezesha wananchi wenye sifa stahiki wakiwamo watumishi wa umma na wafanyakazi katika sekta binafsi kutumia haki yao ya Kikatiba kupiga kura.

#StarTvUpdate

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *