Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy atakuwa mmoja wa watakaohudhuria mkutano huo wa kilele.

Katika taarifa, afisi ya Starmer imesema mwito wake huo atakaoutoa katika mkutano huo uliopewa jina “muungano wa walio na nia” unalenga kuhakikisha kuwa Ukraine imekuwa na mwendelezo wa mafanikio iliyoyapata wiki hii katika uwanja wa mapambano.

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kujihami ya NATO Mark Rutte, Waziri Mkuu wa Denmark Mette Frederiksen na mwenzake wa Uholanzi Dick Schoof wanatarajiwa pia kuhudhuria mkutano huo wa kilele London huku viongozi wengine akiwemo rais wa Ufaransa Emmanuel Macron wakitarajiwa kujiunga kwa njia ya mtandao.

Wandani wa ukraine wiki hii wameiwekea Urusi shinikizo zaidi huku Marekani ikitangaza vikwazo vikali dhidi ya sekta ya mafuta ya Urusi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *