Bao la Fenerbahce lilifungwa na Kerem Aktürkoglu kupitia mkwaju wa penalti katika dakika ya 34 ya mechi, baada ya Angelo Stiller kumuangusha Milan Skriniar. Hii ni mechi ya pili mfululizo Stuttgart kufungwa katika mashindano hayo.

Kocha wa stuttgart Sebastian Hoeness amesema wanatoka huko Uturuki wakiwa wanajivunia kwa mchezo mzuri walioucheza kwani ndivyo walivyopanga kucheza licha ya kuwa hakuweza kupata pointi tatu muhimu.

Fenerbahce ambao wanafunzwa na kocha raia wa Ujerumani Domenico Tedesco, kwa sasa wana jumla ya pointi sita baada ya kupata ushindi katika mechi yao iliyopita walipochuana na Dinamo Zagreb.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *