Marcus Rashford

Chanzo cha picha, Getty Images

Mshambuliaji wa Manchester United Marcus Rashford, 27, anataka kusalia Barcelona ambako anacheza kwa mkopo wa msimu mzima katika klabu hiyo ya Uhispania, ambayo ina chaguo la kumsajili mchezaji huyo wa kimataifa wa Uingereza kwa mkataba wa kudumu mwishoni mwa msimu. (ESPN)

Manchester United wako tayari kusawajili viungo wawili wapya mwaka 2026, huku mchezaji wa kimataifa wa Brazil mwenye umri wa miaka 21 Andrey Santos akiwa miongoni mwa wachezaji sita wanaoteuliwa akiwemo Carlos Baleba, 21, wa Brighton na Cameroon . (Talk sport)

Mshambulizi wa Newcastle United na Ujerumani Nick Woltemade, 23, bado ana matumaini ya kuichezea Bayern Munich katika siku zijazo. (Bild – kwa Kijerumani)

Beki wa kati wa Crystal Palace na England Marc Guehi, 25, ni mmoja wa wachezaji wanaolengwa na klabu ya Bayern Munich ya Ujerumani katika safu ya ulinzi, pamoja iwapo mchezaji wa kimataifa wa Ufaransa Dayot Upamecano, 26, hataongeza mkataba wake au iwapo Kim Min-jae wa Korea Kusini atauzwa. (Sky Sports Ujerumani)

Everton wako tayari kumsajili tena mshambuliaji wa Brazil Richarlison, baada ya Tottenham kuonyesha nia ya kutaka kumuuza mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 mwezi Januari. (TeamTalk)

Mshambuliaji wa Uholanzi Joshua Zirkzee anataka kuondoka Manchester United katika usajili la Januari, huku West Ham wakiongoza mbio za kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24. (Miroor)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *