Katika mahojiano aliyoyafanya na gazeti la Time mnamo Oktoba 15 na ambayo yalichapishwa jana, Trump ameionya vikali Israel akisema uvamizi hauwezi kufanyika kwasababu hiyo ndiyo ahadi aliyoitoa kwa mataifa ya Kiarabu.

Matamshi haya ya Trump yanakuja wakati ambapo waziri wa mambo ya kigeni wa marekani Marco Rubio ameonyesha imani kuwa usitishwaji mapigano uliosimamiwa na Marekani utaendelea kudumu.

Marekani bado inasalia kuwa muungaji mkono mkubwa wa Israel kijeshi na katika masuala ya kidiplomasia.

Mnamo Jumatano, wabunge wa Israel walipitisha miswada miwili ya uvamizi wa Ukingo wa Magharibi, hatua iliyolaaniwa na Makamu wa Rais wa marekani JD Vance aliyekuwa Israel hapo jana.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *