
Baada ya kuwasili katika mji mkuu wa Kiev, Reiche amewaambia waandishi wa habari kwamba katikamsimu huo wa baridi, watafanya kila wawezalo kuhakikisha Ukraine inajikimu vyema.
Amesema watasaidia kujenga upya miundombinu ya nishati na kubadilisha vifaa vilivyoharibiwa pamoja na kikosi kazi chake kifedha na kiutaratibu, kwa ushirikiano wa karibu na wasambazaji wa nishati wa Ujerumani na Ukraine.
Urusi yashambulia kwa makusudi mifumo ya nishati ya Ukraine
Ameongeza kuwa tangu mwanzo, Urusi ililenga kwa makusudi mifumo ya usambazaji ya nishati ya Ukraine katika jaribio la kuwahujumu raia wake. Reiche amesema Ujerumani pia itatoa fedha za ziada kwa ajili ya ununuzi wa gesi asilia.