Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendelealo (Chadema), Tundu Lissu amefikishwa tena katika Mahakama Kuu leo Oktoba 24, 2025 ikiwa ni mwendelezo wa kesi ya uhaini inayomkabili.

Lissu alivyofikishwa tena Mahakama Kuu

Kwa mujibu wa hati ya wito wa kufika mahakamani iliyopelekwa kwa pande zote, kesi hiyo imepangwa kusikilizwa mfululizo kuanzia Oktoba 6, mpaka leo Oktoba 24, 2025.

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendelealo (Chadema), Tundu Lissu akiwa chini ya ulinzi wakati akiwasili katika Mahakama Kuu leo Ijumaa Oktoba 24, 2025. Picha na Ally Mlanzi.

Lissu anakabiliwa na shtaka moja la uhaini kinyume na kifungu cha 39(2) (d) cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu, linalotokana na maneno aliyoyatamka kuhusiana na kuzuia kufanyika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.

Jopo la mawakili wa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendelealo (Chadema), Tundu Lissu wakiwa katika Mahakama Kuu leo Ijumaa Oktoba 24, 2025. Picha na Ally Mlanzi.

Endelea kufuatilia Mwananchi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *