Waangalizi wa Uchaguzi kutoka Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) wamezindua rasmi safari za kuelekea katika mikoa mbalimbali ya Tanzania, kwa ajili ya kufuatilia maandalizi na mwenendo wa Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba 29 mwaka huu.

Ujumbe huo unaongozwa na aliyewahi kuwa Makamu wa Rais wa Uganda, DkT. Specioza Kazibwe, ambaye ameahidi kuwa timu yake itashirikiana kwa karibu na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) pamoja na wadau wengine kuhakikisha uchaguzi unakuwa huru, wa haki na wenye amani.

Mhariri | @claud_jm

#AzamTVUpdates

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *