
Rais aliyepo madarakani Alassane Ouattara, mwenye umri wa miaka 83, anawania muhula wa nne, hatua itakayopanua utawala wake hadi karibu miongo miwili.
Maelfu ya wafuasi wake walijitokeza mjini Abidjan, ambapo aliwahakikishia ushindi akisema, “Mbwa wanabweka lakini msafara tayari umesonga.”
Wagombea wa upinzani, akiwemo Simone Gbagbo, mke wa rais wa zamani Laurent Gbagbo, na Jean-Louis Billon, waziri wa zamani wa biashara, pia walifanya mikutano yao ya mwisho.
Wagombea wawili waondolewa kwenye kinyang’anyiro
Uchaguzi huu unakuja huku wagombea wawili wakuu wa upinzani, Laurent Gbagbo na Tidjane Thiam, wakiondolewa kwenye kinyang’anyiro — hali iliyosababisha maandamano na hofu ya vurugu.
Shughuli mjini Abidjan zimepungua kwa hofu ya ghasia, huku wachambuzi wakisema Ouattara ana nafasi kubwa ya kushinda katika raundi ya kwanza.