Matamshi ya Merz kuhusu wahamiaji yameibua maandamano ya karibu kila siku katika miji mikubwa.

Baadhi ya asilia 63% ya watu waliohojiwa katika utafiti uliofanywa na shirika la habari la ZDF, wamesema wanakubaliana na matamshi ya kansela huku 29% wakisema wanapinga.

Baadhi ya Wajerumani wasema hawajashuhudia matatizo yoyote

Hata hivyo, ni asilimia 18 pekee ya waliohojiwa waliosema kuwa wakimbizi wanasababisha matatizo katika maeneo yao huku asilimia 74 ikisema hawajakumbana na matatizo yoyote makubwa ama kutoshuhudia kabisa.

Wiki iliyopita, Merz alisema serikali yake inarekebisha makosa yaliopita katika sera ya uhamiaji na inapiga hatua.

Hata hivyo Merz amesema bado wana shida ya jinsi miji yao inavyoonekana na ndio sababu waziri wa mambo ya ndani wa nchi hiyo anawezesha na kutekeleza shughuli kubwa ya kuwarejesha wahamiaji hao makwao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *