
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Ndani, Marjana Rewa, amesema shambulizi hilo lilitokea wakati askari wa ulinzi wa mpakani alipokuwa akimhoji mtuhumiwa huyo kuhusu utambulisho wake katika mkoa wa Zhytomyr, kaskazini-magharibi mwa nchi.
Kwa mujibu wa taarifa za awali, mlipuko huo uliwaua askari huyo, mtuhumiwa na abiria wengine wawili. Sababu ya tukio hilo bado haijabainika.
Sheria ya kijeshi bado yatumika Ukraine
Polisi wamesema mshukiwa mwenye umri wa miaka 23 alikamatwa hivi karibuni akijaribu kuondoka nchini kuelekea magharibi. Ukraine bado ipo chini ya sheria ya kijeshi, inayowazuia wanaume wenye umri kati ya miaka 22 na 60 kuondoka nchini bila kibali rasmi.