YANGA vs SILVER STRIKERS: “Tunatakiwa kuishambulia hii timu, hatuna muda wa kukaa nyuma”

YANGA vs SILVER STRIKERS: “Tunatakiwa kuishambulia hii timu, hatuna muda wa kukaa nyuma”
Kocha wa Yanga, Patrick Mabedi amesema siku zote kwenye mchezo wa mpira wa miguu, presha haikosekani na jambo la msingi ni kujua namna gani unakabiliana na hali hiyo.

Mabedi anasema kesho katika dimba la Benjamin Mkapa, hawatokwenda kuzuia, watashambulia zaidi.

Mabedi anasema mashabiki ni wachezaji wa 12 na kesho wanawahitaji sana ili wachezaji waweze kutekeleza vema majukumu yao.

Kwa upande wa nahodha msaidizi wa Yanga Dickson Job anasema mashabiki walale leo wakiuwaza mchezo wa kesho na kujitokeza uwanjani.

(Imeandikwa na @allymufti_tz)

#CAFCL #Yanga

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *