YANGA vs SILVER STRIKERS: “Tupo kwenye hasara ya kuongozwa kwa goli moja…, kwahiyo tuna mlima wa kupanda, ni mlima mrefu, lakini...

YANGA vs SILVER STRIKERS: “Tupo kwenye hasara ya kuongozwa kwa goli moja…, kwahiyo tuna mlima wa kupanda, ni mlima mrefu, lakini ukiifikiria Young Africans unapata matumaini kwamba Yanga wanaupanda huu mlima”

Meneja Habari na Mawasiliano wa Yanga SC, Ally Kamwe amesema wanajua ugumu wa mechi yao dhidi ya Silver Strikers baada ya kutanguliwa kwa goli moja.

Kamwe anasema wakiitazama Yanga yao, wanapata matumaini kwamba mlima huo wataweza kuupanda kwa maana ya kuvuka na kuingia hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL).

Mechi itapigwa saa 11:00 jioni na LIVE AzamSports3HD.

Imeandaliwa na @jairomtitu3
Mhariri: @allymufti_tz

#Yanga #Kamwe

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *