#HABARI: Marekani imemuwekea vikwazo Rais wa Colombia Gustavo Petro, wakidai alishindwa kuzuia biashara haramu ya dawa za kulevya ambapo vizuizi hivyo pia vinamuathiri mke wake na mtoto wake mkubwa wa kiume.
“Rais Petro ameruhusu magenge ya dawa za kulevya kushamiri na kukataa kuyazuia,” alisema Waziri wa Hazina ya Marekani Scott Bessent.
Mbali na familia ya rais, Marekani pia iliweka vikwazo kwa Waziri wa Mambo ya Ndani wa Colombia Armando Benedetti na watu waliowekewa vikwazo watashindwa kuzifikia mali zao zilizopo Marekani.
Colombia hapo awali ilichukuliwa kuwa mshirika wa Marekani katika mapambano dhidi ya dawa za kulevya, ikipokea mamia ya mamilioni ya dola kila mwaka kutoka Washington, ili kuimarisha vikosi vyake vya kijeshi.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
📱Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 📱kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.