#HABARI: Serikali kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa kushirikiana na taasisi isiyo ya Serikali ya Elico Foundation imeikabidhi Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa, soko la kuuzia samaki na mtambo wenye thamani ya Milioni 129.98 kwa ajili ya kukaushia dagaa ikiwa na uwezo uliosimikwa wa kukausha mazao hayo kwa wastani wa tani 3 hadi 5 kwa siku, mradi ambao umelenga kuongeza uzalishaji wa mazao hayo yenye kuathiriwa na changamoto ya hali ya tabia ya nchi ambao ulipelekea uchakataji wa zao hilo kuwa duni.
Akizungumza katika hafla ya uzinduzi na kukabidhi mtambo huo, leo Oktoba 24, 2025, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dkt. Edwin Mhede amesema Sekta ya Uvuvi imekuwa ikikabiliwa na upotevu mkubwa wa mazao ya uvuvi baada ya kuvunwa, hasa kwa dagaa ambao mara nyingi huharibika kutokana na kukaushia chini, na wakati mwingine mazao hayo hukutana na mchanga, matope, au mvua, na hivyo kupunguza ubora wake, bei yake sokoni na hata kuathiri afya za walaji.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
📱Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 📱kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.