Katika ujumbe uliochapishwa kwenye mtandao wa Telegram, kamandi ya jeshi la Ukraine imesema kuwa takriban wanajeshi 100 wa Urusi wameuawa na wengine kutekwa wakati wa mashambulizi ya kukikomboa kijiji hicho.

Hata hivyo taarifa hii haijaweza kuthibitishwa kwa njia huru.

Torske ni kijiji kaskazini mwa mkoa wa Donetsk. Kabla ya kuanza kwa vita, zaidi ya watu 1,000 waliishi katika eneo hilo lakini sasa kimeharibiwa pakubwa.

Torske imetekwa na kukombolewa mara kadhaa

Muda mfupi baada ya vita kuanza, kijiji hicho kilitekwa na wanajeshi wa Urusi na baadaye kukombolewa na wale wa Ukraine wakati wa mashambulizi ya mwaka 2022. Hivi karibuni, kiliangukia tena mikononi mwa Urusi.

Kijiji hicho ni muhimu kwa sababu ya nafasi yake kwenye kilima kwenye ukingo wa mto Zherebets ambayo huunda kizuizi cha asili na kufanya kuwa vigumu kwa wanajeshi kusonga mbele kuelekea Lyman.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *