Kutokana na sifa hiyo, jiji hilo limezoeleka kwa mishe mishe zake za kila siku. Hata hivyo, baadhi ya wakazi wake ambao ni wananchi wa kipato cha chini, hasa wachuuzi na wafanyabiashara ndogo ndogo wanakiri kwamba, katika kipindi hiki cha kampeni kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, biashara imepungua.

Muhsin Seif, ni muuza mahindi ya kuchoma jijini humo katika eneo la Mnara wa Saa, “Ni kweli hali halisi kidogo kumepooza pooza kutokana na Uchaguzi, wengi wapo katika pirika pirika za Uchaguzi.

Nae Henry Magessa, anayejishughulisha na usafirishaji, anasema wanaendelea kufanya biashara lakini sio kama ilivyokuwa awali.

“Tunafanya biashara japo mzunguko sio mzuri kama zamani. Labda kwa sababu ya hizi kampeni labda zinaweza kuwa zimechangia kwa sababu wengi tuliokuwa tunawapa huduma hivi sasa hawapo.”

Wakati huo huo, waandishi wa habari wa TRT Afrika, ambao wapo jijini humo kufuatilia matukio mbalimbali nchini humo, wamekiri kwamba, hali ya jiji kidogo imezizima, tofauti na siku za kawaida ambapo kunakuwa na msongamano mkubwa wa magari.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *