Mkataba, huo ambao utaanza kutumika baada ya kuidhinishwa na mataifa 40, unatarajiwa kuwianisha ushirikiano wa kimataifa,

ushirikiano dhidi ya uhalifu mtandaoni, lakini pia umekosolewa na wanaharakati na makampuni ya teknolojia juu ya wasiwasi wa uwezekano wa ukiukwaji wa haki za binadamu.

Uhalifu wa mitandaoni wasababisha hasara kubwa katika jamii

Wakati wa sherehe ya ufunguzi wa mkutano huo, katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres, amesema mitandao imekuwa nafasi inayotumiwa na wahalifu kila siku kulaghai familia, kuiba riziki za watu pamoja na kupora mabilioni ya dola kutoka kwa chumi za mataifa.

Kwa upande wake, Rais wa Vietnam Luong Cuong, amesema kusainiwa kwa mkataba huo, kunathibitisha kudumishwa kwa ushirikiano wa mataifa mengi kwa ajili ya maslahi ya pamoja ya amani, usalama, utulivu na maendeleo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *