Mwanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Lulu Mapunda, amewasihi wananchi pamoja na wafuasi wa chama hicho kut…Mwanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Lulu Mapunda, amewasihi wananchi pamoja na wafuasi wa chama hicho kut…

Mwanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Lulu Mapunda, amewasihi wananchi pamoja na wafuasi wa chama hicho kutoandamana tarehe 29 Oktoba, siku ya Uchaguzi Mkuu, na badala yake kujitokeza kwa wingi kupiga kura kwa amani.

Lulu ametoa wito huo leo Oktoba 25.2025 alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari mkoani Tanga, ambapo amesisitiza umuhimu wa kudumisha utulivu na kuepuka vitendo vyovyote vinavyoweza kusababisha vurugu au umwagaji wa damu huku akisema wanaohamasisha maandamano wao wapo Nchini za nje hivyo wananchi wawapuuze.

Amesema kuwa njia bora ya kuonyesha uzalendo na kutetea demokrasia ni kwa wananchi wote kutumia haki yao ya kikatiba ya kupiga kura kwa amani, badala ya kushiriki maandamano ambayo yanaweza kuhatarisha usalama wa watu na mali.

Aidha, amewataka vijana kutokuwa sehemu ya uchochezi au vitendo vya uvunjifu wa amani, akisisitiza kuwa taifa linahitaji utulivu ili maendeleo yaweze kuendelea kupatikana.

#StarTvUpdates

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *