Dar es Salaam. Kizazi cha sasa kimeamka tofauti kabisa! Hawa siyo wale vijana wa zamani waliotamani kuwa pairoti, daktari au mhandisi. Hawa wa leo hii vijana wengi hutamani kuwa influencers! Yaani, si kazi, si ofisi, ni simu, kamera na folowazi!

Kama huamini, muulize kijana yeyote wa mjini, utasikia; “Mimi nataka nicheze TikTok, nifanye content, nifanane na wale wana wanaokula bata na brand kubwa!” Kuanzia mabinti zetu, vijana wetu, waume na wake zetu.

Kwao, kuwa influencer ni life goal. Ni “ajira ya ndoto” inayompatia umaarufu, mashabiki, mkwanja wa haraka na connection kibao. Ndo maana nikisikia wanataka kuzima mitandao najiuliza hao watu wanawaza sawa sawa?

Lakini je, mchezo ni rahisi kama unavyoonekana? Ni safari ndefu na mchezo huanzia na simu. Na simu iwe kali. Wengi wanaanza kidogo tu, video moja ya ujinga TikTok, post ya utani Instagram, au tweet ya ku-trend Twitter.

Ukiona views zikipanda, moyo unacheka! Unasema, “baaaasi nimepata njia yangu ya kutoka kimaisha!” Lakini kumbe nyuma ya likes na comments kuna kazi kubwa, presha kubwa, na maisha ya kujituma kila siku.

Kila mtu anataka kutrendi, hata kama inamaanisha kujidhalilisha kidogo mitandaoni. Na wengine wanafanya mambo ya ajabu tu mradi wapate views, wanatukana, na wengine hujifanya wajuaji wa kila kitu.

“Naona wengine wanakula bata, nami nimekimbia ofisi!” Siku hizi vijana wengi wanaachana na kazi zao za kawaida ili waingie katika game la ushawishi. Wanatemana na michongo ya ajira, kubanana banana na ‘Maechiara’ ofisini.
Wanatamani kuwa huru huruni. Hupenda wakiona influencers wakienda Dubai. 
Wakitwanga photo na kampuni kubwa kubwa, ama kutangaza bidhaa na dilizi za mamilioni ya mkwanja. Macho yao huvutika. Lakini hawajui, nyuma ya kamera kuna mikataba, presha, ushindani mkubwa na misukumo ya kadhia.

Kama huna ubunifu, unazama haraka. Mitandao ni kama bahari, leo unaweza kuwa juu, kesho au mtondogoo ukapotea kabisa!
Sio mila influencer ana hela hela.

Ushawishi umekuwa kama vile sinema. Watu wanaishi maisha ya “Instagram reality”, kila kitu kwao kinaonekana safi, lakini ukweli ni tofauti. Ogopa ‘spotilaiti’ aiseee huwa ina ‘draivu kreizi’.

Kuna wanaoonesha wakila bata mitandaoni, kumbe hata nguo ya show off ni ya kukodi. Kuna wale wanaoonekana matajiri, kumbe wanategemea endorsement moja tu kwa miezi mitatu. Just imagine my friend.

Mitandao imetengeneza presha kubwa ya “kuonekana” badala ya “kuwa halisi.” Hapo ndipo vijana wengi wanapotea. Hukimbizana na taswira badala ya ndoto halisi. Mwisho hupoteza focus na kuishi kwa stress back to back.

Masela na masista duu walianza kujilipua na ngada kwa sababu hizi. Wengine wakaishia kwenye mitungi na kupoteza kabisa kila kitu. Wapo waliotangulia mbele za haki mapema kwa haraka na tamaa ya kutoboa fasta.

Kuna wachache wanaofanikiwa. Tusikosoe tu, wapo walioweza kuigeuza mitandao kuwa maisha. Kazi kama brand ambassadors, kuuza bidhaa, kukrieti content za kuelimisha, na wanapata kipato safi.

Wengine wamefungua kampuni zao, wanatoa ajira, wamegeuza simu kuwa ofisi ya kweli. Na siri yao ni moja tu, ubunifu, nidhamu, na uthubutu. Siyo maneno makali, siyo skendo, bali consistency na maudhui bora.

Hao ndio influencers wa kweli, wanaotumia mitandao kujenga na siyo kubomoa. Na wanapush mikoko ya maana mjini. Wana miliki mijengo mtambuka hata vacation zao ni London, Paris, New York nk.

Kwa kifupi, kizazi hiki kimeingia rasmi kwenye zama za kidigitali. Ushawishi umekuwa ajira, simu imekuwa chombo cha fedha, na jina lako linaweza kuwa biashara.Lakini kabla hujajiingiza, jiulize swali moja tena la msingi.

“Nataka kuwa maarufu, au nataka kuwa mwenye thamani?” Elewa mitandao inaweza kukupa every thing, fame, followers, lakini kama huna akili ya mkwanja, followers hawalipi bili. Utaishia kuwa talk of the town without faranga.

Tunaelekea Desemba, kimsingi ni holiday season na content kali, caption za moto kwa wale wana wanaoishi online. Ila kumbuka bata ni poa, lakini akili mbele ya kamera ni muhimu zaidi! Usikae kindezi ndezi jiongeze.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *