Wagombea wengine wanne pia wako kwenye kinyang’anyiro hicho cha urais nchini Ivory Coast.

Wapinzani wake wawili wakuu ambao ni rais wa zamani Laurent Gbagbo na Tidjane Thiam waliondolewa kwenye kinyang’anyiro hicho.

Ouattara atarajiwa kushinda katika raundi ya kwanza

Waangalizi wanatarajia Ouattara kushinda 50% ya kura zinazohitajika ili kujipatia ushindi katika raundi ya kwanza.

Taifa hilo la Afrika Magharibi, ambalo lina idadi ya watu karibu milioni 33, linakabiliwa na mvutano mkali wa kisiasa.

Upinzani na asasi za kiraia zinalalamika kuhusu vikwazo dhidi ya wakosoaji wa Ouattara na hali ya hofu.

Ukosefu wa ajira kwa vijana na rushwa ni masuala makubwa yalioangaziwa kwenye kampeni.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *