
Akiwahutubia waandishi wa habari hii leo Jumamosi, Reiche amesema ilikuwa hali ya hofu kwake, lakini cha kusikitisha ni kwamba hali hiyo ni sehemu ya maisha ya kila siku kwa raia wa Ukraine.
Ameongeza kuwa usiku huo umemdhihirishia wazi kwamba mashambulizi ya Urusi dhidi ya watu wa Ukraine yalilenga kuwadhoofisha.
Takriban watu wawili wameuawa na wengine 12 kujeruhiwa katika shambulio hilo.
Mashambulizi dhidi ya miundombinu ya nishati ya Ukraine ni hatari
Akiwa Kiev hapo jana Ijumaa, Reiche alisema mashambulizi dhidi ya mifumo ya kusambaza umeme na nishati muda mfupi kabla ya kuanza kwa majira ya baridi ni hatari.
Ameahidi msaada kwa Ukraine kujenga upya miundo mbinu ya nishati yake iliyoharibiwa na akaongeza kuwa Ujerumani haitawaacha watu wa Ukraine.
Reiche aliwasili Ukraine jana Ijumaa na ujumbe wa kiuchumi kwa ziara ya siku kadhaa.