
Katika ujumbe alioandika kwenye mtandao wa X, Rubio amesema hawatawasahau mateka waliofariki chini ya kuizuizi cha wanamgambo wa Hamas.
Saa chache kabla ya kuhitimisha ziara yake ya siku tatu nchini Israel, Marco Rubio amesema amekutana na familia za raia wa Marekani Itay Chen na Omer Neutra na kuongeza kwamba hawatapumzika hadi mabaki yao na ya wengine yatakaporejeshwa.
Kundi la Familia za Mateka na Waliopotea, limepongeza matamshi ya Rubio, likisema mateka 13 wanahitaji kurejea nyumbani.
Pia limemshukuru waziri huyo wa mambo ya nje wa Marekani na kumtaka aendeleze mikakati hadi mwili wa mateka wa mwisho utakaporejeshwa nyumbani.