Chanzo cha picha, Getty Images
Chelsea inaweza kuokoa pauni milioni 52 ikiwa haitamsajili beki wa kati wa Ufaransa Dayot Upamecano hadi msimu ujao wa joto atakapokuwa mchezaji huru, lakini kuna hatari ya kumkosa mchezaji huyo wa miaka 26 iwapo Bayern Munich itamuuza Januari, huku Liverpool ikiwa miongoni mwa vilabu vinavyomtaka. (Football.London)
Licha ya kiungo wa kati wa Sporting, Denmark, Morten Hjulmand, 26, kuwa na kifungu cha kutolewa cha pauni milioni 70, Manchester United wana imani kwamba wanaweza kumpata kwa takriban pauni milioni 50. (Teamtalk)
Manchester United pia inamfuatilia kiungo wa kati wa Bayern Munich na Ujerumani Aleksandar Pavlovic, 21. (Caught Offside)
Chanzo cha picha, Getty Images
Real Madrid wako tayari kulipa euro milioni 100 (pauni milioni 87) ili kumsajili mshambuliaji wa Uturuki mwenye umri wa miaka 20, Kenan Yildiz kutoka Juventus. (Fichajes)
Fulham inaongeza juhudi za kukubaliana mkataba mpya na meneja Marco Silva na kumzuia bosi huyo wa Ureno kuondoka mwishoni mwa msimu. (Football Insider)
Manchester City, Chelsea na Manchester United ni miongoni mwa vilabu vinavyomtaka winga wa Cologne Mjerumani Said El Mala, mwenye umri wa miaka 19. (Sport1)
Chanzo cha picha, Getty Images
Mshambuliaji wa Brazil Gabriel Jesus, 28, anataka kubaki Arsenal angalau hadi mkataba wake wa sasa utakapoisha Juni 2027. (ESPN)
Mkataba wa mkopo wa Crystal Palace na Getafe kwa mshambuliaji wa Nigeria mwenye umri wa miaka 22 Christantus Uche utakuwa wa kudumu tu ikiwa atacheza mechi 10 au zaidi. (Sport)