
Akiwa ndani ya ndege ya rais wa Marekani, Air Force One, Trump amewaambia waandishi wa habari kwamba anatarajia kuwa na mkutano mzuri na Xi huku akitumai kwamba China itaingia katika makubaliano ya kuepusha ushuru zaidi wa asilimia 100 ambao unafaa kuanza Novemba 1.
Trump anatarajiwa kufanya ziara Malaysia na Japan
Trump anatazamiwa kukutana na Xi nchini Korea Kusini katika siku ya mwisho ya ziara hiyo ya kikanda katika jitihada za kusaini makubaliano ya kumaliza vita vya kibiashara kati ya nchi hizo mbili zenye uchumi mkubwa duniani.
Wakati wa ziara yake hiyo ya kwanza barani Asia tangu arejee madarakani mwezi Januari, Trump pia anatarajiwa kufanya ziara nchini Malaysia na Japan.